Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC, Onesmo Olengurumwa akiambatana na Mratibu THRDC- Zanzibar Bw. Abdallah Abeid hii Leo wamekutana kwa mazungumzo pamoja na kuutambulisha Ofisi ya THRDC Zanzibar kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, sheria, utumishi na Utawala bora, Waziri Haroun Ali Suleiman.

Katika mazungumzo yao waratibu THRDC wamepata wasaha wa kumualika na kumkaribisha rasmi Waziri Suleiman katika Uzinduzi wa Ofisi za THRDC unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao visiwani Zanzibar.

Hata hivyo Waziri Haroun amewashauri waratibu kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Idara ya Utawala ambayo imekuwa ikihusika Moja kwa Moja na masuala ya Haki za Binadamu visiwani Zanzibar. Lakini pia Waziri Suleiman ameahidi kutoa ushirikiano kwa Mtandao katika shughuli ya uzinduzi Ofisi zake unaotarajiwa kufanyika visiwani humo.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, THRDC wenye wanachama takribani 200 Tanzania Bara na Visiwani umekuwa ukifanya Kazi kuhakikisha Watetezi wa Haki za Binadamu wanakuwa na mazingira salama ya ufanyaji Kazi lakini pia kushirikiana na Mamlaka mbali mbali za Serikali ili kuhakikisha wananchi wanafikiwa katika maswala ya Haki za Binadamu Nchini.

Imetolewa na

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Octoba 29,2021