Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa akiambatana na Mratibu THRDC Zanzibar, Bw. Abdallah Abeid wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar kwa mazungumzo na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP, Mohamed H. Hassan

Katika Ziara hiyo waratibu wamepata wasaha wa kuutambulisha THRDC- Zanzibar Pamoja na kumkaribisha Kamishna katika uzinduzi wa Ofisi za THRDC – Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao visiwani Zanzibar.

Hata hivyo katika mazungumzo hayo THRDC imefanikiwa Kujadiliana namna ya kuendeleza utolewaji wa Mafunzo mbali mbali kwa Jeshi la Polisi katika maswala ya Haki za Binadamu na Utawala bora kwa lengo la kukuza uzingatiwaji wa Haki za Binadamu Nchini.

Tangu kuanzishwa kwake THRDC imekuwa ikifanya Kazi kwa kushirikiana na jeshi la Polisi katika maeneo mbali mbali ikiwemo Utoaji wa mafunzo, shughuli za Mtandao Pamoja na kuhakikisha Watetezi wa Haki za Binadamu wanafanya Kazi katika mazingira salama wakati wote.

Imetolewa na

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Octoba 10,2021