THRDC NA UNIC WAENDESHA MDAHALO KUWAELIMISHA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MCHIKICHINI KUHUSU KAZI ZAO

Dar es Salaam – Tanzania

Leo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) pamoja na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) wameitembelea shule ya Sekondari Mchikichini iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, kuwaelimisha wanafunzi wa shule hiyo kuhusu dhana ya Utetezi wa Haki za Binadamu, kazi za THRDC pamoja na kazi za Umoja wa Mataifa na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Sustainable Development Goals).

THRDC iliwakilishwa na James Laurent – Afisa Habari na Kavazi la THRDC wakati UNIC iliwakilishwa na Didi Nafisa ambaye ni Afisa Habari wa UNIC Kitaifa.

Mdahalo huo mfupi uliandaliwa na Klabu ya Utunzaji Mazingira ya Shule ya Sekondari Mchikichini inayoitwa Roots & Shoots.

Mwisho wa mdahalo huo ulifwatiwa na kipindi cha maswali na majibu kwa wanafunzi pamoja na chemshabongo. Pichani ni baadhi ya matukio katika mdahalo huo asubuhi ya leo.

[envira-gallery id=”5724″]

Imetolewa leo tarehe:
26 Septemba 2019

Na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)