Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa hii leo ametembelea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) iliyopo Jijini Dodoma.

Mazungumzo baina ya Mratibu THRDC na Mwenyekiti wa Tume ambaye pia ni Jaji mstaafu, Mathew P. M. Mwaimu, Mratibu THRDC yamelenga zaidi kuangalia maeneo ya kuongeza Mashirikiano katika uwanda wa Haki za Binadamu mjadala ambao umeonyesha Kuwa na mwelekeo mzuri katika kuleta Matokeo chanya kwa Haki za Binadamu Nchini.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC umekuwa na mashirikiano ya karibu na Tume (THBUB) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 na umekuwa na mkataba wa makubaliano (MoU) wa kuhakikisha Kazi za Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania zinatambuliwa na kuthaminiwa lakini pia kuhakikisha ulinzi wa Haki za Binadamu na Utawala Bora unaonekana na kuheshimiwa.

Imetolewa na

Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu
28 Septemba, 2021