Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) hii leo unaendesha mafunzo ya siku mbili kwa wanawake mawakili wa haki za binadamu takribani 40 kuhusu namna ya kuendesha mashauri yenye maslahi ya umma (Public Interest Litigation).Mafunzo ambayo yanayofanyika jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo ambayo yanaanza hii leo Septemba 3,2021 yatahitimishwa rasmi hapo kesho na mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania,Jaji Joaquine De-mello.

Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo mawakili wanawake kuhusu namna ya kuendesha mashauri yenye maslahi ya umma,na kuongeza idadi ya mawakili wanawake katika kuendesha mashauri hayo.

Miongoni mwa wawezeshaji katika mafunzo hayo ya siku mbili ni Wakili Onesmo Olengurumwa,Mratibu THRDC,Mhe.Profesa Jaji Mstaafu Justice Ruhangisa,Wakili Nuru Maro,Afisa Uchechemuzi kutoka THRDC na Wakili Prisca Chogero kutoka AVC &Partners Advocates,Jaji Mstaafu Robert Makaramba na Wakili Magdalena Rwebingira.

Pia mawakili wanawake katika mafunzo haya wataongezewa uelewa juu ya umuhimu wa mashauri ya kimkakati kama njia moja wapo ya kufanya uchechemuzi kuhusu mabadiliko ya sheria pamoja na kutambua kesi mbalimbali ambazo zinaweza kufunguliwa katika mahakama za ndani na za kimataifa.

Imetolewa
Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
3/9/2021