Je, wewe ni Binti Mtetezi wa Haki za Binadamu na ungependa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani pamoja nasi???

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeandaa Chakula cha Jioni cha pamoja (Dinner Gala) siku ya Jumapili tarehe 8 Machi 2020, ambapo Watetezi Vijana wa Kike wataweza kukutana na Wanawake Watetezi Mahiri na Wakongwe kwenye sekta ya Asasi za Kiraia nchini kupata ujuzi na kujadili maswala mtambuka kuhusu Utetezi wa Haki za Wanawake nchini na duniani.

Kushiriki, tafadhali tutumie HISTORIA YAKO FUPI YA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU pamoja na MAJINA YAKO KAMILI na NAMBA YAKO YA SIMU ili tuweze kukutumia Mwaliko rasmi.

 

Wasiliana nasi kupitia;
• Barua Pepe: advocacy@thrdc.or.tz

• Simu: +255 769 642 208