TANZIA!!!

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesikitishwa na taarifa za kifo cha BI. GETRUDE ALEX (40) ambaye alikuwa Ofisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Commission for Human Rights and Good Governance – CHRAGG).

Bi. Getrude Alex alifikwa na umauti usiku wa Novemba 23, 2019; siku mbili baada ya kupata ajali maeneo ya Ubungo – Dar es Salaam, mnamo tarehe 21 Novemba, 2019 na kulazwa katika Hospitali ya Muhimbili; kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG).

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa niaba ya wadau wengine wa Haki za Binadamu nchini na wanaAZAKi, tunatanguliza pole kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ambayo ni taasisi ya juu kitaifa katika usimamizi wa haki za Binadamu nchini, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kwa msiba uliowafika.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Getrude Alex mahala pema. Amina!

 

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

Tarehe:
26 Novemba, 2019

 

**(English Translation)**

CONDOLENCE TO THE COMMISSION FOR HUMAN RIGHTS AND GOOD GOVERNANCE (CHRAGG)!!!

The Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) has been saddened by the unfortunate death of MS. GETRUDE ALEX (40) – an officer of the Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG).

According to the Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG), Ms. Gertrude Alex passed away on the night of 23rd November 2019; just two days later following her tragic accident on 21st November 2019 at Ubungo – Dar es Salaam. Ms. Getrude was rushed and admitted at Muhimbili Hospital on the same day.

Therefore, the Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC), on behalf of other human rights stakeholders and the Civil Society sector in Tanzania hereby express our deepest sympathy towards the Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG), relatives and friends of the deceased for their loss.

May her soul rest in eternal peace, Amen!

By:
Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)
Dated: 26th November 2019