Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania( THRDC), umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanachama wa Mtando, Mkurugenzi wa shirika la ELIMISHA Ndugu FESTO SIKAGONAMO MWAKASENGE kilichotokea siku ya tarehe 6 Januari 2022 mkoani mbeya alipokuwa akipatiwa matibabu.

THRDC tunaungana na wote walioguswa na msiba huu mzito na tunatuma salamu za pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki wote.

Enzi za uhai wake Festo alikuwa mwanachama hai wa Mtandao( THRDC) kwa takribani miaka mitatu tangu alipojiunga na Mtandao mwaka 2020, kupitia Shirika lake la ELIMISHA na taaluma yake ya uandishi wa habari Ndugu Festo alipambana kutoa elimu ya kuwawezesha vijana na wanawake kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mafunzo mbali mbali kwa jamii.

Mungu aipumzishe Roho ya marehemu mahali pema peponi.

Imetolewa na;
Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Leo tarehe 7 Januari 2022