
TAARIFA ZA KIFO CHA JAJI MKUU MSTAAFU AUGUSTINO RAMADHANI
Asubuhi hii THRDC imesikitishwa kupokea taarifa za kifo cha Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani majira ya saa 2 katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Wakati wa uhai wake Jaji Mkuu Mastaafu Augustino Ramadhani alikua mtetezi mzuri wa haki za binadamu kabla na hata baada ya kustaafu kwake.
Kwa namna ya kipekee tutamkumbuka marehemu Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani kwa jinsi alivyoisaidia THRDC mara kadhaa katika kutoa mafunzo kwa mawakili wanaosimamia kesi za haki za binadamu nchini.
Tunatanguliza salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, watetezi wa haki za binadamu, wadau wa haki za binadamu, wadau wa mahakama na umma kwa ujumla. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. Amina!
N.B: THRDC itaendelea kutoa taarifa zaidi.
Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Tarehe 28 Aprili 2020
Message *PUMZIKA KWA AMANI JAJI,MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU,