TAARIFA KWA UMMA: THRDC YASAINI MKATABA NA CIVICUS KUIMARISHA UHURU WA KUJIELEZA NCHINI

Leo tarehe 2 Oktoba 2019, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa niaba ya Watetezi TV, umesaini mkataba wa miezi mitatu (Oktoba 2019 – Desemba 2019) wenye thamani ya Dola za Kimarekani USD 20,000/=, sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 50 kutoka shirika la CIVICUS (World Alliance for Citizen Participation). Fedha hizo zinalenga kuiimarisha nafasi ya raia katika ushirikishwaji wao kwenye masuala mbalimbali ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania.

Mradi huu wa miezi mitatu unatarajiwa kuongeza nguvu katika utetezi wa haki za binadamu kwa kuhakikisha upatikanaji wa habari na makala zinazohusu haki za binadamu, kutambua na kuripoti  habari za utekelezaji na utetezi wa haki za binadamu zinazofanywa na watetezi wa haki za binadamu, mashirika na taasisi za serikali na zisizo za kiserikali nchini.

 

Imetolewa na:

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),

Tarehe 2 Oktoba 2019