SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI ZA KIJAMII (WORLD DAY OF SOCIAL JUSTICE)

Leo tarehe 20 Februari ni siku ya kuadhimishwa kwa Haki za Kijamii kimataifa.
Haki za Kijamii ni dhana ya usawa miongoni mwa wanajamii katika umiliki wa mali na fursa mbalimbali bila kujali tofauti za kijinsia, kirangi, kikabila, kiumri, kitamaduni au ulemavu.

Mfano wa haki za kijamii ni pamoja na haki ya kufanya kazi, haki ya kuheshimiwa, haki ya kupata elimu, haki ya maendeleo, haki ya kumiliki rasilimali asili n.k.
#WDSJ2020