Mtandao umeshiriki kikamilifu katika siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu duniani ya mwaka 2014.

Sherehe hizo husherekewa kila mwaka kwa ajili ya kutambua umuhimu wa haki za binadamu, na hufanyika tarehe ambayo azimio la kimataifa la haki za binadamu lilipitishwa yani tarehe 10 December.

Ikumbukwe kuwa azimio la haki za binadamu lililkuja baada ya dunia kushuhudia uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu katika vita ya za kwanza na za pili na hivyo ili kuzuia hali kama hiyo isijitokeze tena azimio la kimataifa liliundwa na kupitishwa mnamo mwaka 1948.

Haki za binadamu kwa siku 135 ndio kauli mbiu ya mwaka huu na inakuja kwa lengo la kutambua kuwa kila siku ni siku ya haki za binadamu na umoja wa mataifa unatambua juhudi za watetezi wa haki za binadamu wanaojitolea kwa moyo ili kulinda haki za binadamu.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) kwa uwezeshaji kutoka kwa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania kwa wameandaa Warsha ya Universal Periodic Review (UPR) katika sherehe hizi za siku ya kimataifa ya haki za binadamu.

Mratibu wa Mtandao Bw. Onesmo Olengurumwa wakati akiwasilisha juu ya Hali ya Watetezi wa haki za Binadamu Nchini alisisitiza kuwa mpango mkakati wa kitaifa wa kutekeleza mapendekezo yaliyokubaliwa na serikali ili kuboresha haki za binadamu katika mkutano wa geneva unatakiwa uwe wazi kwa umma ili ufuatiliaji wa utekelezaji uweze kufanyika vyema.

Aidha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali iliweka bayana kuwa mpango mkakati wa kitaifa ingawa haujawahi kusambazwa kwa sababu moja au nyingine ila sio siri na hivyo mtu yeyote anaweza kuupata akiomba.

Hivi sasa mtandao upo kwenye utengenezaji wa mbinu za kufanya ufuatiliaji ili kutambua utekelezaji wa mapendekezo yaliyokubaliwa na serikali.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.