TANZIA!!!
MWANACHAMA WETU BI. GLADNESS MUNUO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI
Wapendwa wanachama,
Salamu kutoka THRDC!
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) pia umepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Baba Mzazi wa mwanachama mwenzetu, Mkurugenzi wa Shirika la Crisis Resolving Centre Bi. Gladness Munuo kilichotokea jioni ya siku ya jana tarehe 17/4/2020.
THRDC inampa pole Bi. Gladness Munuo pamoja na ndugu jamaa na marafiki zake kwa msiba huu. Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuwasihi wanachama wetu tuungane pamoja kuiombea faraja familia ya Bi. Gladness Munuo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana litukuzwe. Amina!