MRATIBU WA KANDA YETU YA KUSINI AITEMBELEA THRDC KUTOA POLE

MRATIBU WA KANDA YETU YA KUSINI AITEMBELEA THRDC KUTOA POLE

Mapema asubuhi ya leo Agosti 27, 2020, tumetembelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania Ndugu Clemence Mwombeki. Shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania ni ofisi inayoratibu kazi za wanachama wa THRDC waliopo katika Kanda ya Kusini, ikijumuisha mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope to Women and Youth Tanzania Ndugu Clemence Mwombeki amefika kwenye ofisi za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kutoa pole kwa Mratibu Kitaifa Bw. Onesmo Olengurumwa kwa kufungiwa akaunti za benki za THRDC hali iliyopelekea Mtandao kushindwa kufanya kazi zake kwa sasa.

Pichani ni Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) akimkabidhi Ndugu Clemence Mwombeki – Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania baadhi ya machapisho ya Mtandao.

 

Imetolewa na:
Dawati la Wanachama – THRDC,
Agosti 27, 2020