Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania Onesmo Olengurumwa Akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam Baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika Wizara mbali mbali Jijini Dodoma, Olengurumwa amepata wasaha wa kutembelea Shule ya sekondari Dakawa Secondary School iliyopo eneo la Dakawa/Dumila Mkoani Morogoro, Mratibu ni mmoja wa Wanafunzi waliowahi kupata elimu katika shule hii Mwaka 2002- 2004 kwa ngazi ya kidato cha tano na cha sita.

Miaka 17 baadae (Septemba 3, 2021) Mratibu ametembelea tena shule hiyo kusalimia walimu na wanafunzi wa Shule hiyo Pamoja na kujionea maendeleo ya shule hiyo.

Hata hivyo baada ya kuwasili katika shule ya Dakawa, Mratibu amekutana na Harambee ya kuchangia katika ujenzi wa fensi imara na ya Kisasa kuizunguka shule hiyo ambayo kwa kiasi wazazi tayari wameonyesha nia ya kushiriki, hivyo shule ikaonelea vyema kuwashirikisha wanafunzi waliosoma katika shule hiyo ili kwa Pamoja kuweza kuimarisha ulinzi katika shule hiyo ambayo awali ilikuwa ya Mchanganyiko (wavulana na Wasichana) Hadi mwaka 2006 ilipobadiliahwa na kwa sasa ina wasichana pekee.

Katika kushiriki kutatua changamoto hiyo Mratibu ameahidi kushawishi wanadarasa wenzie wa mwaka 2004 kuchangia kiasi cha shilingi Milioni 1 au zaidi ili kufanikisha azma hiyo huku akiahidi kushirikisha baadhi yau wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo kuhakikisha shue hiyo iafikia malengo yake.

“Nawashauri wote ambao walipata wasaha wa kusoma katika shule ya Dakawa kushiriki katika harambee hii ya ujenzi wa fensi ya shule kama njia Mojawapo ya kuienzi shule yetu” Mratibu Olengurumwa

Hata hivyo Mratibu alipata wasaha wa kukutana na wanafunzi wa shule ya Dakawa, kujitambulisha, kuzungumza na kuwashauri wanafunzi kusoma kwa bidii na kuendelea Kuwa na nidhamu Ili waweze kutimiza malengo yao, pia amewaahidi kuendelea kushirikiana na shule na kuangalia uwezekano wa kuwa na klabu ya Haki za Binadamu shuleni hapo.

Walimu wa Dakawa wamemshukuru Mratibu kwa kukumbuka na kutembelea shule hiyo na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha wanafunzi wanatimiza ndoto zao kwa kupata elimu bora na hitajika.

Imetolewa
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu
3 Septemba, 2021