MRATIBU THRDC AKUTANA NA KATIBU MKUU WA TEC FR. KITIMA

Dar es Salaam, Tanzania

Leo tarehe 24 Juni 2021, Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Bw. Onesmo Olengurumwa alitembelea ofisi za Tanzania Episcopal Conference (TEC), zilizopo jijini Dar es salaam, na kukutana na Katibu Mkuu wa TEC, Fr. Kitima kwa ajili ya maongezi mafupi.

Bw. Olengurumwa alitumia nafasi hii kumkaribisha rasmi Fr. Kitima kama muwakilishi wa TEC, na kumuelezea kwa ufupi juu ya siku kubwa ya maadhimisho ya watetezi wa haki za Binadamu Tanzania.

Moja ya majadiliano ni pamoja na namna ya Mtandao kushirikiana na taasisi za kidini katika kutekeleza Mpango Wa AZAKI wa Utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa miaka mitano wa Maendeleo ya Taifa ambao unatarajiwa kuzinduliwa siku ya maadhimisho ya mwaka wa 7 wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini.

Ikumbukwe ya kwamba, asasi za kidini zimekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za kijamii nchini kama vile elimu, maji na afya kwa miaka mingi sasa.

Maadhimisho ya siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania yanategemea kufanyika siku ya Ijumaa, Julai 2, 2021, jijini Dar es Salaam.

Taasisi zingine za kidini zilizoalikwa ni pamoja na Baraza Kuu la Waisilamu Tanzania (BAKWATA) na Christian Council of Tanzania (CCT).

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
24 Julai 2021.