MRATIBU KITAIFA WA THRDC ATEMBELEA OFISI YA MRATIBU WA KANDA (Zonal Coordinating Unit) YA MTANDAO, UNGUJA

MRATIBU KITAIFA WA THRDC ATEMBELEA OFISI YA MRATIBU WA KANDA (Zonal Coordinating Unit) YA MTANDAO, UNGUJA

Unguja, Zanzibar

Leo Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Bw. Onesmo Olengurumwa ametembelea ofisi ya uratibu wa kanda ya mtandao (Zonal Coordinating Unit), kwa kanda ya Unguja Zanzibar. Ofisi hiyo inajulikana kwa jina la “Zanzibar Fighting Against Youth Challenges Organization (ZAFAYCO)”, ambao pia ni wanachama hai wa THRDC.

Kati ya mambo mengi yaliyojadiliwa kupitia ugeni huo ilikuwa pamoja na hali ya watetezi wa haki za binadamu kwa upande wa Zanzibar, na jinsi gani ofisi ya Mtandao kwa upande wa Zanzibar utarutubisha utetezi wa haki za binadamu visiwani Zanzibar.

Pichani ni Mratibu Kitaifa wa THRDC akiwa na Mkurugenzi wa ZAFAYCO, Bw. Abeid Abdalla alipotembelea ofisi ya ZAFAYCO visiwani Zanzibar.

Imetolewa leo:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Julai 29, 2021.