MRATIBU KITAIFA WA THRDC AFANYA MAJADILIANO NA MRAJISI ZANZIBAR

MRATIBU KITAIFA WA THRDC AFANYA MAJADILIANO NA MRAJISI ZANZIBAR

Unguja, Zanzibar

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Bw Onesmo Olengurumwa pia ametembelea ofisi ya Mrajisi na kufanya majadiliano mafupi na Mrajisi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Bw. Ahmed Kherlid.

Bw. Olengurumwa amemtembelea Mrajisi Bw. Ahmed Kherlid leo Alhamisi, tarehe 29 Julai 2021 na kujadili mambo mengi pamoja na utaratibu wa kufungua ofisi ya THRDC kwa upande wa Zanzibar. Ofisi hii italenga kuratibu wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzanua (THRDC) wanaofanya kazi za utetezi wa haki za Binadamu visiwani Unguja na Pemba.

Ugeni huo ulikua wa kheri sana na mrajisi alifurahi na kuonesha ushirikiano mkubwa kwa THRDC.

Imetolewa na;
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Tarehe 29 Julai 2021.