Shirika mwanachama la Morogoro Paralegal Centre (MPLC) leo hii imeshiriki katika uzinduzi wa kituo cha huduma ya Mkono kwa Mkono kwa wanaofanyiwa ukatili wa Kijinsia katika Manispaa ya Morogoro.

Kituo hicho kimejengwa na Sawa Wanawake Tanzania kwa Ufadhili ChildFund Korea. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 7 Februari 2022, ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Morogoro, DC Albert Msando.

Katika picha ni DC Albert Msando akikata utepe wa kituo hicho kilichozinduliwa, huku akiwa na wawakilishi kutoka sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo Asasi za Kiraia.

#Miaka10YaTHRDC
#10YrsOfTHRDC