Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu leo tarehe 16 mwezi wa tatu mwaka 2015 umeendesha mkutano wa gafla kwa Asasi za kiraia kwa ajili ya kuweza kujadili masuala la usalama wakati wa uchaguzi. Mkutano huo umeudhuriwa na wawakilishi wa mashirika zaidi ya kumi na tatu.

Mkutano umelenga masuala ya usalama kwa waangalizi wa uchaguzi nchini pamoja na usalama wa kazi zao, Mtandao katika mkutano huo umetoa tamko la kuzisihi asasi za kiraia kuzingatia usalama wa waangalizi wa uchaguzi pale waendapo katika kazi za uangalizi.

Suala la uangalizi kwa waangalizi wa uchaguzi limekua ni suala la muhimu sana hasa baada ya kuvamiwa na kupigwa kwa waangalizi wa uchaguzi wa TACCEO waliokuwa wakiangalia uandikishwaji wa kwenye daftari la kudumu wa Biometric Voters Registration (BVR).

Kuvamiwa na kutekwa kwa waangalizi hao ndio kumeamsha ari ya asasi nyingi na kuzifanya zihofie usalama wao.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.