MGAWANYIKO KWENYE JAMII BADO NI CHANGAMOTO KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI

Arusha – Tanzania

Mgawanyiko kwenye jamii unaohusishwa na maslahi binafsi umetajwa kuwa ni kikwazo kwa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini.

Akielezea mafanikio na changamoto katika shughuli za Utetezi wa Haki za Binadamu nchini, Ndugu Lebaraka Laizer
ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Maasai Pastoralists Development Organization (MPDO-LARETO) amesemema kwamba wamekuwa wakikumbana na mgawanyiko huo ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakiungana na wale ambao wanatuhumiwa kudhulumu Haki za wananchi kwa maslahi binafsi.

Mbali na changamoto hizo Ndugu Lebaraka Laizer ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kutoa taarifa za kila mwaka pamoja na kulipa ada ya uanachama.

[envira-gallery id=”5875″]

Pichani ni Mkurugenzi wa shirika la Maasai Pastoralists Development Organization Ndugu Lebaraka Laizer pamoja na Mratibu Kitaifa wa THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa, Afisa wa Dawati la Wanachama – THRDC Bi.Joyce Elizer na Mratibu wa Kanda ya THRDC ya Kaskazini Ndugu Erick Luwongo.

Pia Mratibu wa Kanda ya THRDC ya Kaskazini Ndugu Erick Luwongo amemkabidhi Ndugu Lebaraka Diary zetu za mwaka 2020 pamoja na majarida ya mwisho wa mwaka 2019.