MAADILI KATIKA VYOMBO VYA HABARI:

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unahudhuria mjadala wa maadili katika vyombo vya habari ulioandaliwa na Internews-Tanzania kupitia mradi wa Boresha Habari.

Mjadala huo unafanyika katika ofisi za Internews zilizopo kinondoni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wahariri, Wanahabari, Wahadhiri kutoka vyuo tofauti tofauti, wawakilishi na Wakurugenzi kutoka Taasisi mbalimbali.

Mjadala umeanza na utambulisho kutoka kwa wadau waliohudhuria na utangulizi uliotolewa na Mkurugenzi wa Boresha Habari, Wency Mushi ambaye alitoa nafasi kwa mjumbe wa kwanza Bwana Jesse Kwayu kuanza kuwasilisha mada inayosema “Ni kwa namna gani Mazingira ya sasa yanachangia kuongeza au kupunguza thamani ya Uandishi wa Habari”.

THRDC inawakilishwa na Msimamizi wa Watetezi TV, Loveness Muhagazi kwa niaba ya Mratibu wa Mtandao huo, Bw. Onesmo Olengurumwa.