Shirika mwanachama la Mtandao, linaloitwa KOK Foundation limefanya hafla ya wanafunzi wa shule ya msingi katika Shehia ya Kangani, Mkoani Pemba.

Hafla hiyo iliongozwa na mgeni rasmi Dr. Mohamed Khamis Mjaka ambae ni makamu mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya Shehia ya Kangani. Wanafunzi waliofaulu zaidi michepuo na kipawa maalum wamezawadiwa vifaa vya masomo kama vile madaftari, sare za shule, na fedha taslim jumla ya shilingi laki sita na elfu thelathini (tsh 630,000).

Pamoja na zawadi hizo, KOK Foundation imewaahidi wanafunzi hao kuwasaidia gharama za shule iwapo zitawashinda.

Mtandao una mashirika wanachama zaidi ya 30 yanayojihusisha ya masuala ya kutetea haki za watoto na elimu.

#Miaka10YaTHRDC
#10YrsOfTHRDC