Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umefurahi kupokea ugeni mzito kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) leo hii, Alhamisi 26th August 2021.

Ugeni huu ni sehemu ya ziara ya Tume ya kutembelea AZAKI zenye makubaliano ya kufanya kazi pamoja zilizo katika mkoa wa Dar Es Salaam. Ambapo wageni kutoka Tume waliofika ni Mheshimiwa Kamishna Nyanda Shuli, Bw. Francis Luziga (Afisa Uchunguzi Mkuu), na Bi. Nancy Ngula (Afisa Uchunguzi Mwandamizi) kutoka ofisi ya Tume ya Daresalaam.

Katika ugeni huu, CHRAGG na THRDC wamejadiliana mambo kadhaa yanayoweza kudumisha mashirikiano yao, pamoja na kudumisha na kuimarisha Haki za Binadamu nchini Tanzania, na masuala mazima ya Utawala Bora.

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
26 Agosti 2021