Shirika mwanachama la Igniting Young Minds Tanzania (IYMT), lililojikita kwenye masuala ya vijana (afya na uchumi), limefanya majadiliano na wadau mbalimbali na serikali juu ya magonjwa ya UVIKO 19 na HIV.

Wakiwa mkoani Shinyanga, IYMT imefanya majadiliano na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, wahudumu wa Afya kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga, Afisa dawati la jinsia mkoani humo, pamoja na wawakilishi kutoka makundi maalum, juu ya matokeo ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO 19 katika jamii sanjari, na kujua namna ambavyo jamii inaendelea kupambana na ugonjwa huo.

Majadiliano hayo ni ya siku mbili, ikiwa leo ni hitimisho la majadiliano, lakini ni mwanzo wa mapambano hai ya pamoja juu ya janga hili la UVIKO 19.

#Miaka10YaTHRDC
#10YrsOfTHRDC