IDRIS SULTAN AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Hatimaye, jana Jumatano jioni tarehe 27 Mei 2020, mchekeshaji Idris Sultan aliachiwa huru kwa dhamana ya polisi baada ya kusomewa mashitaka mawili pamoja na mwenzake Innocent Maiga:

1) Kushindwa kusajili SIM CARD ambayo ilikuwa na umiliki wa mtu mwingine.

2) Kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki wa SIM CARD hiyo.

 

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Tarehe 28 Mei 2020