ERICK KABENDERA’s CASE ADJOURNED, BUT DIAGNOSED WITH SPINAL PROBLEMS

ERICK KABENDERA’s CASE ADJOURNED, BUT DIAGNOSED WITH SPINAL PROBLEMS

Dar es Salaam – Tanzania

Today on 18th September 2019, Tanzanian investigative journalist Erick Kabendera who is facing three charges including; Leading an Organized crime, Evading Tax and Money Laundering, has yet again had his case adjourned by the Kisutu Resident Magistrate Court in Dar es Salaam to October 1, 2019 next month. Public prosecutor Wankyo Simon told the court today that, the investigation into Kabendera’s case is still underway, but at an advanced stage.

However, journalist Kabendera told the court that he had been admitted to Amana hospital (following the court’s order) yesterday for medical examination including X-RAY tests after previously informing the court about his deteriorating health. “Preliminary tests have shown that I have spinal problems. Further tests have been taken to examine whether there are other complications. Medical test results will be out by the end of this week, though I’m still experiencing severe back pains”; said Kabendera before the court today.

On the other hand, THRDC’s Advocate Jebra Kambole representing Erick Kabendera, has also urged the Public Prosecutor to speed up the investigation into his client’s case.

It should be recalled that, Investigative Journalist Erick Kabendera has been behind bars since 29th July 2019 when he was arrested at his Mbweni Residence in Dar es Salaam-Tanzania.

(Swahili translation)

KESI YA KABENDERA YAAHIRISHWA TENA, AKUTWA NA MATATIZO YA MGONGO

Dar es Salaam – Tanzania

Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari Erick Kabendera imeahirishwa tena hadi tarehe Mosi Oktoba mwaka huu. Wakili wa serikali Wankyo Saimon ameieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua nzuri.

Hata hivyo, Erick Kabendera ameiambia Mahakama kuwa, hapo jana alichukuliwa vipimo katika hospitali ya Amana na kimojawapo kilikuwa kipimo cha X-RAY.

“Vipimo vya awali vimeonesha kuwa nina matatizo ya mgongo, ila wamechukua vipimo vingine ili kuweza kutambua kama kuna matatizo mengine. Majibu yatatoka mwishoni mwa wiki hii lakini bado napata maumivu makali ya mgongo”; amesema Kabendera.

Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Jebra Kambole ameuomba upande wa Serikali kuendelea kuharakisha upelelezi wa shauri hilo.

Shauri hilo namba 75 la Mwaka 2019 limeahirishwa hadi Oktoba Mosi 2019 litakapotajwa tena.

Ikumbukwe kuwa, Kabendera anashitakiwa kwa makosa matatu ya; Utakatishaji Fedha, Kujihusisha na Genge la Uhalifu na Kukwepa Kulipa Kodi. Na alikamatwa nyumbani kwake mnamo Julai 29, 2019.

#FreeErickKabendera
#JusticeForKabendera