🗞NEWS ALERT!

BOLLEN NGETTI IS NOT AT STAKISHARI POLICE STATION

Following reports about the arrest of investigative journalist Mr. Bollen Ngetti, yesterday on 8th August, 2019, Advocate Jones Sendodo from the Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) went to Stakishari police station to follow up on the matter as it was claimed that he was being detained at that police station.

However, the Advocate has reported that the journalist is not at the said police station after going through the station’s logbook three times and not finding his name.

The advocate is heading to the central police station in attempts to know what’s happening and where journalist Bollen Ngetti is being held at, so as to offer him legal representation which is his right.

 

🗞HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE!

BOLLEN NGETTI HAYUPO KITUO CHA POLISI STAKISHARI:

Kufuatia taarifa za kukamatwa kwa mwandishi wa habari za uchunguzi, Bollen Ngetti, hapo jana tarehe 08/08/2019, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) @thrdcoalition ulimtuma wakili wake Jones Sendodo, kufuatilia katika kituo cha polisi Stakishari ambapo ilisemekana kuwa mwandishi huyo alipelekwa.

Hata hivyo wakili huyo ametoa taarifa kuwa Mwandishi huyo hayupo katika kituo hicho baada ya kupitia daftari la majina ya watuhumiwa bila kuona jina lake.

Wakili huyo sasa anaelekea kituo cha polisi kati (Central police station) kuendelea kufuatilia na kufahamu kituo kinachomshikilia.