AFYA YA KABENDERA YAZOROTA KIZUIZINI:

Wakili Jebra Kambole kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) anaesimamia kesi ya mwandishi wa habari, Erick Kabendera, ameiambia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kuwa hivi karibuni afya ya Kabendera imekuwa ikizorota. Wakili Jebra ameitaarifu mahakama kwamba tangu usiku wa tarehe 21 Agosti 2019, Kabendera amekuwa akipata shida kupumua usiku na miguu yake kukosa nguvu. Ameomba mahakama itoe amri kwa askari magereza wampeleke Kabendera hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

THRDC kwa sasa inawasiliana na maafisa wa gereza la Segerea ili kuhakikisha kwamba masuala ya afya ya Erick yanapata matibabu haraka.

Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera anaendelea kuteseka kizuizini akishtakiwa kwa makosa yasiyo na dhamana, huku upande wa mashtaka wa Serikali ukidai kuwa uchunguzi bado haujakamilika.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Dar es Salaam,
30 Agosti, 2019

(English Translation)
KABENDERA’s HEALTH DETERIORATES IN DETENTION:

The Tanzania Human Rights Defenders Coalition advocate representing journalist Erick Kabendera, Jebra Kambole, has told the Kisutu Resident Magistrate court during the session today that recently Kabendera’s health has been deteriorating. Adv. Jebra informed the court that since the night of 21st August 2019, Kabendera has been having difficulties breathing at night and his legs have been weak. He has requested the court to order the prison wardens to take Kabendera to Muhimbili National hospital for medical procedures.

THRDC is currently communicating with officials at Segerea prison to ensure that Erick’s health issues get immediate medical attention.

Investigative journalist Erick Kabendera continues to suffer in detention; charged with unbailable offenses, while the prosecution side still claims that the investigation is still incomplete.

#FreeErickKabendera

Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC),
Dar es Salaam,
30th August, 2019