UN YATANGAZA KUFUTA MATUKIO KANDO YA BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU (HRC) HUKO GENEVA SHAURI YA HOFU YA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA VIRUSI VYA KORONA (COVID-19)

Geneva – Uswisi

Siku ya tarehe 2 Machi 2020, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Geneva (UNOG) alituma barua kwa Rais wa Baraza la Haki za Binadamu kuhusu hali ya ugonjwa wa COVID-19 na athari yake kwa vipindi vya awamu ya 43 vya Baraza la Haki za Binadamu(HRC) vinavyoendelea kufanyika.

Baada ya kupokea barua hiyo, Rais wa HRC ameripotiwa kuendesha kikao cha dharura na Ofisi kujadili hali hii ya Kimataifa.

Raisi wa HRC amesema kuwa kulingana na ratiba nzito ya kongamano na mikutano ya 2020, kuahirisha vipindi vinginevyo vya awamu 43 ya HRC vitaleta changamoto kubwa. Amehimiza kuwa, badala ya kutafuta suluhisho litakalohusisha kufutwa kwa matukio yote ya kando, au walau yale yanayofanyika sehemu iliyofungwa, wawakilishi washiriki kwenye vipindi kupitia mkutano wa video.

Vipindi vya awamu ya 43 ya Baraza la Haki za Binadamu vilianza mnamo tarehe 24 Februari 2020 na vinatarajiwa kuisha tarehe 20 Machi 2020, hivyo bado vipindi vinaendelea kwa sasa.

 

Imetolewa na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Tarehe 3 Machi, 2020